MAKUBALIANO YA KUSAIDI SEKTA YA KILIMO KATI YA TADB NA PASS YAFIKIWA

D3 Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Kushoto) akizungumza kabla ya kutiliana saini makubaliano yatakayowezesha wakulima wanaokopa TADB kupata dhamana kutoka PASS. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa PASS, Bw. Nicomed Bohay.D6Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Kushoto) akitia saini makubaliano yatakayowezesha wakulima wanaokopa TADB kupata dhamana kutoka PASS. Katkati ni Mkurugenzi Mkuu wa PASS, Bw. Nicomed Bohay na na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa PASS, Bw. Killo Lussewa (Kulia).

D8Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Kushoto) akibadilishana hati za makubaliano yatakayowezesha wakulima wanaokopa TADB kupata dhamana kutoka PASS na Mkurugenzi Mkuu wa PASS, Bw. Nicomed Bohay (Kulia).

D9Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa PASS, Bw. Nicomed Bohay (Kulia) wakionesha hati za makubaliano yatakayowezesha wakulima wanaokopa TADB kupata dhamana kutoka PASS katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya TADB.

D5Wanahabari wakiwajibika wakati wa hafla ya kuwekeana saini makubaliano kudhamini mikopo kwa wakulima wanaokopa TADB.

………………………………………………………………………………………………

Na Mwandishi Wetu,

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa kushirikiana na Mfuko wa Kusaidia Kilimo (PASS) wameingia makubaliano ya kudhamini mikopo kwa wakulima wasio na dhamana watakaokopa kupitia TADB.

Wakizungumza katika hafla ya kuwekeana saini makubaliano hayo, yaliyofanyika katika Ofisi za TADB, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi na Mkurugenzi Mkuu wa PASS, Bw. Nicomed Bohay wamesema kuwa katika kukabiliana na changamoto za ukosefu wa dhamana za uhakika kunakochagiza ukosefu wa upatikanaji wa mikopo kwa wakulima taasisi hizo zimekubaliana kuwawekea dhamana wakulima wenye sifa ya kukopesheka katika Benki hiyo ila wanakosa dhamana waweze kudhaminiwa na PASS.

Bw. Samkyi amesema pamoja na umuhimu wa Sekta ya Kilimo, bado ukuaji wa sekta hiyo umekuwa ukikabiliwa na changamoto mbali mbali kama vile kiwango kidogo cha uzalishaji; Ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa; riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo; mikopo ya muda mfupi; masharti magumu ya kukopa bila kuzingatia hali halisi ya sekta ya kilimo  na mazao ambayo inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

“Makubaliano yetu ya leo, ni ya kihistoria katika kilimo cha nchi yetu kwa kuwa yataongeza idadi ya wakulima wanaokopesheka kuongezeka na hivyo kuchangia kufikia malengo ya TADB ambayo ni kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini Tanzania na kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini,” amesema Bw. Samkyi.

Bw. Samkyi ameongeza kuwa TADB ikiwa ni Benki Kiongozi katika utoaji wa mikopo katika sekta ya kilimo ina wajibu wa kuchochea kuinua uzalishaji wenye tija katika Sekta ya Kilimo kwa kuendeleza miundombinu muhimu, mathalani: skimu za umwagiliaji, usafirishaji, hifadhi ya mazao, usindikaji, na masoko ili kuchagiza kufikia malengo ya Mpango wa Pili wa Maendeleo unaojielekeza kwenye viwanda.

“Kama Benki Kiongozi  ya maendeleo ya kilimo, pamoja na kuhamasisha mabenki na taasisi nyingine za kifedha kutoa fedha kwenye mnyororo mzima wa kilimo, tuna furaha leo kuweza kupata washirika wataowawekea dhamana wakopaji wetu hivyo kukidhi matakwa ya kisheria kama yalivyowekwa na Benki Kuu ya Tanzania,” alisema.

Bw. Samkyi ameongeza kuwa kwa kushirikiana na Serikali, wabia wa kimkakati na wadau wengine katika kuendeleza sekta ya kilimo,  hasa kuboresha na kutekeleza na juhudi zozote sera zinazohusiana na kuhisha ushiriki wa wananchi kwenye mifumo ya kifedha. Na pia watatumia fursa hiyo kuhamasisha upatikanaji wa fedha zenye masharti nafuu na endelevu, ili kuinua ushiriki wa wakulima wadogo katika mfumo wa kifedha pamoja na kuhamasisha kilimo cha kisasa na cha kibiashara kwa wakulima wadogo wadogo.

Kwa upande wake Bw. Bohay amesema kuwa kwa kuanzia PASS itatoa dhamana yenye thamani ya shilingi bilioni tatu (3) na zitakuwa zikiongezeka kadri maombi ya wateja itakavyoongeza.

“Leo tunafarijika kufikia makubaliano na TADB ambao kimsingi ni wadau wetu wakuu kwa kuwa sote tumeanzishwa na Serikali pia tuna lengo kuu moja la kimsingi ambalo ni kuinua ukuaji wa sekta ya kilimo ili kuchagiza ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania,” alisema Bw. Bohay.

Kwa mujibu wa Bw. Bohay tangu kuanzishwa kwake PASS imeshawekea dhamana mikopo ya zaidi Bilioni 314 ambayo imewafikia wakulima zaidi ya 323,000 nchini kote.

Kwa upande wa TADB licha ya uchanga wake imeshakopesa zaidi ya bilioni moja kwa vikundi nane (8) vyenye jumla ya wakulima wadogo wadogo 857, ambavyo vimetimiza vigezo mpaka sasa huku ikishughulikia maombi mengine. Ambapo kwa mujibu wa Bw. Samkyi kabla ya kutoa mikopo hiyo, benki inawatembelea na kutoa elimu kwa wakulima jinsi ya kuimarisha vikundi vyao, ambapo jumla ya vikundi 89 vyenye jumla ya wanakikundi 21,526 vimefikiwa mpaka sasa.

TADB ilianzishwa kwa Sheria Namba 5 ya mwaka 2006 inayosimamia Benki na Taasisi za Fedha, pamoja na Kanuni za Uanzishaji wa Benki na Taasisi za Fedha (Development Finance) za mwaka 2012. Lengo la msingi la kuanzishwa kwa TADB ni kutoa mikopo ya muda mfupi, kati na muda mrefu kwa sekta ya kilimo ili kuleta mapinduzi ya kilimo nchini

About

Hello, I am a regular author. To edit this text edit your profile in Users area of admin.