TTB YAKUTANA NA WADAU WA UTALII

 

UT1Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania, Bi. Devota Mdachi akiongea na wadau wa Utalii katika ukumbi wa mikutano wa Bodi ya Utalii Tanzania.

UT2Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Utalii Tanzania, Bw. Richard Rugimbana akitoa maelezo katika moja ya mada zilizoongelewa kwenye mkutano huo. Aliyekaa upande wa Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Hoteli Tanzania, Bi Latifah Sykes pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Boari ya Utalii Tanzania, Bi. Devota Mdachi.

UT3Wengine ni Baadhi ya wawakilishi kutoka vyama mbalimbali vya utalii Tanzania waliyohudhulia ni Bw. Laurence Paul (Katikati) ambaye ni Katibu Mtendaji wa Chama cha Waendesha Safari za Anga Tanzania, kulia kwake ni Bw.Moses Ngereza wa  Shirikisho la Utalii Tanzania na Bi E. Fernandes waTASOTA  

UT4Washiriki wote wa mkutano huo.

…………………………………………………………………..

Bodi ya Utalii Tanzania imekutana na wadau wa Utalii wa Tanzania kwa lengo la kujadili namna watakavyoweza kushirikiana katika kutangaza utalii wa Tanzania. Mkutano huo uliohudhuliwa na viongozi wa vyama mbalimbali vya utalii vya Tanzania;  Shirikisho la Utalii Tanzania (TCT), Chama cha Wamiliki wa Hoteli Tanzania (HAT),  Chama cha Waendesha Safari za Anga Tanzania (TAOA) na Chama cha Mawakala wa Utalii Tanzania (TASOTA)

Aidha, katika mkutano huo wadau waliweza kutambulishwa tovuti maalumu (Tourism Destination Portal), ulioandaliwa na TTB kwa ajili ya kuboresha utangazaji wa utalii kupitia TEHAMA. Tovuti hiyo inapatikana kwenye http://www.tanzaniatourism.com/en.

Mkutano huo ulifanyika tarehe 20/04/2016 katika ukumbi wa mikutano wa Bodi ya Utalii, Dar Es Salaam.

About

Hello, I am a regular author. To edit this text edit your profile in Users area of admin.