USAFI DAR SIO NGUVU YA SODA TENA: MIKAKATI YAIMARISHWA

 

????????????????????????????????????

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akiongozana na Diamond Plutnamz huku ulinzi ukiwa umeimarishwa wakati wa matembezi hayo yaliyofanyika leo kwa ajili ya kuhamasisha wakazi wa jiji la Dar es salaam kufanya usafi katika maeneo yao.????????????????????????????????????Haya ni miongozi mwa matukio yaliyojiri wakati wa matembezi hayo ya kuhamashiwa wakazi wa jiji kufanya usaifi ambapo kampeni maalum ya siku 90 za kufanya usafi zimezinduliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda.

????????????????????????????????????

????????????????????????????????????

Wapiga picha waliendelea na ubunifu wa kutafuta picha nzuri kama wanavyoonekana hapa kwenye picha wakiwa kwenye pikipiki wakipiga picha katika matembezi hayo.

????????????????????????????????????

Baadhi ya washiriki wa matembezi hayo wakifanya mazoezi mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam ambako ndiko kampeni hiyo ilikozinduliwa.

????????????????????????????????????

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akishiriki katika mazoezi hayo mara baada ya mtembezi hayo kuwasili katika viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es salaam.

????????????????????????????????????

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akisalimiana na viongozi wa dini waliofika katika uzinduzi wa kampeni hiyo ambao ni Sheikh Mkuu wa Dar es salaam Sheikh  Alhadi Mussa Salim na  Askofu  David  Mwasota kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally  Hapi????????????????????????????????????Kikundicha ngoma kikitumbuia katika uzinduzi huo

12Kundi la Yamoto Band likitumbuiza katika zunduzi huo.

13

14Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo wakiwa katika viwanja vya Leaders Kinondoni.

15Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh. Sophia Mjema, Askofu David Mwasota, Sheikh Mkuu wa Dar es salaam Alhadi Mussa Salum na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi wakiwa katika uzinduzi huo.

16Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika kwenye viwanja vya Leaders mara baada ya matembezi ya kuhamasisha wananchi kufanya usafi katika maeneo yao.

IMG_6078Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam wa pili kutoka kushoto na wenyeviti wa wenyeviti wa mitaa kutoka wilaya zote tatu wakifanya ishara ya kufangia ikiwa ni uzinduzi rasmi wa siku 90 za kufanya usafi katika jiji la Dar es salaam kutoka kulia ni Juma Ngemwa Kinondoni, Mbayo Chuma Ilala na Bakiri Makere Temeke.

IMG_6086Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi akizungumza katika uzinduzi huo na kutoa maagizo kwa watendaji na watumishi wa Manispaa ya Kinondoni kuhakikisha wanazingatia na kutimiza malengo kuhakikisha Kinondoni inakuwa safi

????????????????????????????????????

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi na Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti Radio Clods Bw. Ruge Mutahaba na Mwanamitindo Millen Magesse ambaye pia ameshiriki kikamilifu katika kampeni hiyo

………………………………………………………………………………………………….

Na. Immaculate Makilika-MAELEZO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amezindua kampeni ya usafi ya mkoa iliyofanyika katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

Kampeni  ya usafi ya  siku 90 inayobeba kauli mbiu “usijifanye mstaarabu kuwa mstaarabu” itaanza kesho (1/5/2016)  kwa lengo la  kuboresha hali ya usafi  katika  mitaa mbalimbali pamoja na  jiji la Dar es salaam kwa ujumla,  ambapo itasaidia kuzuia magonjwa ya mlipuko, na wakazi wa jiji hilo wamehamasishwa kushiriki kufanya usafi katika mitaa yao pamoja na maeneo mbalimbali na baadae washindi  kupatiwa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni 100 kwa mitaa miwili itakayokuwa imeshinda, ambapo pia  Mkuu huyo wa mkoa aligawa vifaa vya usafi kwa wenyeviti wa mitaa kutoka wilaya zote tatu za Kinondoni, Ilala na Temeke.

Bw. Makonda amesema kuanzia sasa wakazi wa jiji la Dar es salaam watafanya usafi katika mitaa na maeneo yao  kila siku ya jumamosi kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 3:00 asubuhi, na baada ya siku 90 washindi wawili, ambapo  mtaa utakaokuwa msafi na wenye makazi yaliyo katika mpangilio mzuri utapata zawadi ya fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 50 na mtaa utakaokuwa msafi lakini hauna makazi yaliyo katika mpangilio mzuri nao utapata fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 50, vilevile  mtaa utakaoongoza kwa uchafu utatangazwa ikiwa ni pamoja na mwenyekiti wake kueleza namna ambavyo ameshindwa  kusimamia usafi katika eneo lake.

“Mganga Mkuu wa Mkoa atafanya ukaguzi na kutangaza  vigezo vya washindi baada ya siku 90, tangu kuanza kwa kampeni hii, tunataka kuona mabadiliko na watu lazima washiriki kwa usafi na kuyapaka rangi  majengo yao. Suala la usafi si la Serikali pekee ni letu sote” alisema Makonda.

Aidha, ameagiza wamiliki wa vyombo vya usafiri kwa Mkoa wa Dar es Salaam hasa daladala kuwa na vifaa vya kutupia taka katika vyombo vyao na kuanzia mei 2, atakayekiuka agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.

Mkuu huyo wa Mkoa ametoa wito kwa kampuni, taasisi na watu mbalimbali kuunga mkono zoezi hilo kwa kutoa misaada mbalimbali ikiemo kuhamasisha wananchi juu ya suala hili. Pia amewapongeza wakazi wa mkoa huo kwa kushiriki kwa wingi katika uzinduzi wa kampeni ya usafi na  kuzipongeza  kampuni za Clouds Media group, Azam na redio ya EFM kwa michango yao katika kufanikisha kampeni hiyo ya usafi kwa mkoa wa Dar es salaam.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi, amewasisitiza wakazi wa  mkoa  wa Dar es salaam kufanya zoezi la usafi kuwa endelevu kwa kuwa wananchi wenyewe ndio wazalishaji wakubwa wa uchafu hivyo ni lazima wahahikishe wanauondoa.

Naye, Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Huria Bw. Mustafa Mkama, amesema wanafunzi wa vyuo mbalimbali wanaunga mkono kampeni hii na kuitaka jamii kwa ujumla ibadilike kwa kufanya usafi na Serikali nayo ihakikishe inaweka vyombo vya kuhifadhia taka  katika maeneo mbalimbali, sambamba na kuendelea kuelimisha wananchi umuhimu wa kuwa na  mazingira safi.

Uzinduzi wa kampeni ya usafi ya mkoa  wa Dar es Salaam ulitanguliwa na maandamano ya Mkuu wa Mkoa, viongozi mbalimbali wa dini na vyama vya siasa, wasanii mbalimbali akiwemo msanii wa muziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul maarufu kama Diamond platnamz pamoja na wakazi wa mkoa huo, ambayo yalianza   katika wilaya za Temeke, Ilala na Kinondoni  na kuishia katika viwanja vya Leaders.

Ikumbukwe  kuwa 9 desemba 2015, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe  Magufuli alihairisha shamrashamra za sherehe za Muungano na kufanya usafi, huku akiwataka watanzania wote kushiki kufanya usafi katika maeneo yao na kuagiza kuwa zoezi la kufanya usafi kuwa endelevu nchi nzima

About

Hello, I am a regular author. To edit this text edit your profile in Users area of admin.